Ruka hadi maudhui
TAKUN
MiundoKazi zanguMauzoMwongozoMsaada
/
FARAGHA

Sera ya faragha

Kwa maneno rahisi: kazi yako ni yako, na tunailinda.

01

Kazi yako ni yako

Akaunti yako inahifadhi tu kile unachoweka mwenyewe: kurasa zako, sherehe na mialiko yako, na — ukitumia TUNZA MAUZO YAKO — bidhaa na mauzo yako. Kwa wageni wako tunahitaji jina tu na kama mwaliko ni wa mtu mmoja au wawili. Hatuombi namba za simu, barua pepe wala vitambulisho vya wageni au wateja wako.

02

Nani anaona nini

Rasimu zako, sherehe zako, orodha za wageni na rekodi zako za mauzo ni zako. Ukurasa wa biashara au wasifu unaonekana kwa umma tu baada ya wewe kubonyeza “Chapisha”, na unaweza kuuondoa hewani wakati wowote. Wateja wanaotembelea ukurasa wako hawaoni mauzo, gharama wala stock yako. Wasaidizi wa sherehe na wanatimu wa mauzo wanaona tu kile ulichowaruhusu, kila mmoja kwa akaunti yake.

03

Usalama wa TAKUN

Ili TAKUN iendelee kufanya kazi vizuri na tuweze kukusaidia unapotuomba, timu ya TAKUN inaweza kufungua akaunti kupitia njia ya usimamizi iliyolindwa kwa hatua mbili za kuingia, na kila ufunguaji unaandikwa. Hakuna mtu anayeweza kuona nenosiri lako.

04

Kufuta taarifa za wageni

Siku saba baada ya sherehe (saa za Tanzania), tunafuta majina ya wageni, misimbo, rekodi za kuingia na picha ya sherehe. Tunabaki na takwimu za jumla tu (idadi ya mialiko, nafasi na walioingia). Kabla ya hapo unaweza kupakua orodha yako ya wageni. Mialiko uliyokwisha kupakua au kutuma haiwezi kufutwa kwenye simu za watu wengine.

05

Kinachobaki

Akaunti yako, kurasa zako za biashara na wasifu pamoja na picha zake, na rekodi zako za mauzo zinabaki hadi utakapozifuta wewe au utakapotuomba tufute akaunti yako. Historia ya mauzo haifutwi kimya kimya: mauzo yaliyokosewa yanafutwa kwa sababu iliyoandikwa.

06

Nenosiri na usalama

Hatuwezi kuona nenosiri lako. Ukilisahau, tunakutumia link ya kuweka jipya. Tunakataa manenosiri yaliyowahi kuvuja mtandaoni. Picha za kurasa zako zinahifadhiwa kwa faragha na kuonyeshwa kupitia link za muda mfupi.

07

Huduma tunazotumia

TAKUN inatumia huduma za kuhifadhi na kuingia (pamoja na Google ukichagua kuingia kwa Google). Tunajua tu ni mara ngapi kurasa zinafunguliwa — bila jina lako, namba ya simu wala mahali ulipo. Hatuuzi taarifa zako, hatuweki matangazo, na hatutumii taarifa za wageni au mauzo kwa kitu kingine chochote.

08

Kufuta akaunti au kuuliza

Wasiliana nasi kwa WhatsApp +255619470497 au simu +255619470497 / +255746474232, kila siku 07:00–19:00 (saa za Tanzania), tukusaidie kufuta akaunti au kujibu swali kuhusu taarifa zako.

Wasiliana nasi · Imesasishwa 2026

TAKUN

Biashara yako. Kazi zako. Sherehe yako.

Msaada kwa wateja

Tunajibu kila siku 07:00–19:00 (saa za Tanzania). Unaweza kutuandikia au kupiga wakati wowote.

WhatsApp +255619470497Piga +255619470497Piga +255746474232
MiundoKazi zanguTunza mauzo yakoMwongozoMsaadaFaraghaMasharti
© 2026 TAKUN
MwanzoMiundoKazi zangu