HUDUMA YA 2 · BURE

TUNZA MAUZO YAKO

Jua umeuza kiasi gani na umebakiza bidhaa ngapi. Rekodi mauzo yako na simamia biashara pamoja na timu yako.

Utaombwa kuingia au kujisajili kwanza, kisha utarudi hapa moja kwa moja.

  • Rekodi mauzo

    Chagua bidhaa, andika idadi, angalia jumla na hifadhi. Stock inapungua yenyewe.

  • Bidhaa na stock

    Stock ni idadi ya bidhaa ulizonazo. Ongeza stock, rekebisha kwa sababu, na upate tahadhari zikikaribia kuisha.

  • Ripoti

    Mauzo ya leo, wiki hii, mwezi huu au tarehe unazochagua — na faili la CSV.

  • Marejesho na marekebisho

    Rekodi bidhaa zilizorudishwa au futa mauzo yaliyokosewa. Historia ya asili haifutwi.

  • Timu yako

    Alika hadi watu 9. Kila mmoja anatumia akaunti yake, na wewe unachagua anachoruhusiwa.

  • Ni siri yako

    Mauzo, gharama na stock havionekani kwenye website yako wala kwa wateja. Huhitaji website ili kutumia huduma hii.

Kumbuka

  • Bei ziko kwa shilingi za Tanzania (TZS), kwa namba kamili.
  • Idadi ni vipande kamili — hakuna desimali.
  • Faida ya bidhaa ni kabla ya gharama nyingine kama kodi ya pango, mishahara au usafiri.
  • Mauzo yanahifadhiwa tu ukiwa na intaneti. Hatusemi yamehifadhiwa kabla hayajafika.
  • Madeni, matumizi, kodi na risiti rasmi bado hazipo kwenye huduma hii.