Ruka hadi maudhui
TAKUN
MiundoKazi zanguMauzoMwongozoMsaada
/
MASHARTI

Masharti ya matumizi

Makubaliano mafupi kati yako na TAKUN.

01

Huduma

TAKUN ni bure: mialiko yenye QR code na kupokea wageni, kurekodi mauzo na stock, website ndogo ya biashara, na link ya wasifu. Hakuna malipo, kikapu wala ujumbe wa SMS unaotumwa na TAKUN.

02

Akaunti yako

Tumia barua pepe yako halisi na nenosiri la TAKUN pekee. Usimpe mtu mwingine nenosiri lako — kila msaidizi wa sherehe anatumia akaunti yake.

03

Unachochapisha

Wewe ndiye unayewajibika kwa unachoweka: andika ukweli, tumia picha ulizo na haki nazo, na weka namba zako mwenyewe tu. Tunaweza kuondoa ukurasa unaodanganya, unaovunja sheria au unaotumia jina la mtu mwingine.

04

Mipaka

Kila akaunti: website moja ya biashara, wasifu mmoja, sherehe mbili zinazoendelea, wageni hadi 1,000 kwa sherehe, wasaidizi hadi 9 kwa sherehe, bidhaa/kazi hadi 10 na picha hadi 3 kwa kila moja.

05

Kupokea wageni

Kila mgeni anaruhusiwa kuingia baada ya mpokeaji kuthibitisha. Ukikosea msimbo mara 5 mfululizo, utasubiri dakika 5. Huduma inategemea intaneti; andaa njia mbadala siku ya sherehe ikiwa mtandao ni dhaifu.

06

Mabadiliko

Tunaweza kuboresha TAKUN na masharti haya. Mabadiliko makubwa tutayaeleza kwenye tovuti.

Wasiliana nasi · Imesasishwa 2026

TAKUN

Biashara yako. Kazi zako. Sherehe yako.

Msaada kwa wateja

Tunajibu kila siku 07:00–19:00 (saa za Tanzania). Unaweza kutuandikia au kupiga wakati wowote.

WhatsApp +255619470497Piga +255619470497Piga +255746474232
MiundoKazi zanguTunza mauzo yakoMwongozoMsaadaFaraghaMasharti
© 2026 TAKUN
MwanzoMiundoKazi zangu